Posts

Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika Mkoa wa Songwe: Shirika la IRDO Lajivunia Kuunga Mkono

Image
  Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika mwaka huu yamefanyika kwa kishindo katika Mkoa wa Songwe, yakishirikisha watoto, wananchi, na wadau mbalimbali. Shirika la IRDO lilikuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha tukio hili linafanikiwa na kutoa mchango wake kwa jamii. Katika viwanja vya Shule ya Sekondari Kakoma, wafanyakazi wa Shirika la IRDO pamoja na vijana wanaojitolea katika shirika hili walikusanyika kwa ajili ya kusherehekea siku hii muhimu. Huku wakiwa na furaha na shauku, walishirikiana na watoto na jamii kwa ujumla katika kuhamasisha haki za watoto, elimu bora, na ustawi wa watoto wetu. Katika tukio hili, vijana wanaojitolea katika shirika la IRDO waliweza kuwaelezea wadau na wananchi mbalimbali waliotembelea banda la shirika hilo kuhusu miradi inayotekelezwa na bidhaa zilizozalishwa na wanufaika wa miradi hiyo. Hili lilisaidia kutoa mwanga zaidi juu ya kazi nzuri inayofanywa na shirika katika jamii. 🌟🛍️🌱 Kwa kuzingatia umuhimu wa afya ya wasichana, wafanyakazi wa Shi...
Image
Elimu kwa Jamii: Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nyerere Wapata Mafunzo Kuhusu Ukatili wa Kijinsia, UKIMWI, na Dawa za Kulevya Katika jitihada za kuelimisha na kuhamasisha jamii kuhusu masuala muhimu ya kijamii na kiafya, Shirika la IRDO limefanya shughuli mbalimbali za kuelimisha wanafunzi. Shughuli hizi zilijumuisha igizo, shairi, na elimu ya moja kwa moja kutoka kwa wataalam. Bi. Witness Ndunguru, Afisa Ustawi wa Jamii kutoka shirika la IRDO, alitoa elimu kuhusu maana ya ukatili wa kijinsia, aina zake, na vitendo vinavyoashiria ukatili wa kijinsia. Alifafanua pia sehemu sahihi za kupata msaada kwa waathirika wa ukatili huo. Ujumbe wake ulilenga kuwaelimisha wanafunzi juu ya jinsi ya kutambua na kupambana na ukatili wa kijinsia katika jamii yao. Kwa upande mwingine, Bw. Johnson Samwel Bilingi, Mkaguzi Msaidizi wa Kituo cha Polisi Tunduma, aliongeza kwamba wanaume pia wanaweza kufanyiwa ukatili wa kijinsia na hawapaswi kusita kutoa taarifa. Aliwaasa wanafunzi kwamba ukatili unaweza ku...
Image
Mzumbe Business Day was commemorated on 7th June 2024 at Royal Tughimbe Hotel in Mbeya, City Dr. Simon Chiwanga, Executive Director of the Integrated Rural Development Organization (IRDO) and Chairman of the Songwe River Basin Stakeholders Platform delivered a public lecture on  Youth Empowerment Mzumbe Business Day was commemorated on 7th June 2024 at Royal Tughimbe Hotel in Mbeya City whereby various government and private institutions, companies and student groups as well as talented individual students were invited. More than 500 students and staff from the Department of Business Education attended the event whose main message was on investment and business opportunities in the public and private sector. The Bank of Tanzania, BRELA, Some Microfinace Banks, Feed the Future and several business companies were among the invited institutions that informed the mass about their areas of expertise and opportunities to the youths. During the day, Dr. Simon Chiwanga, Executive Director ...
Image
Mkurugenzi wa Shirika la Uwiano wa Maendeleo Vijijini/IRDO Dr. Simon Chiwanga, ametembelewa na Idara ya Masomo ya Biashara katika Chuo Kikuu Mzumbe Mkurugenzi wa Shirika la Uwiano wa Maendeleo Vijijini/IRDO Dr. Simon Chiwanga, ametembelewa na Idara ya Masomo ya Biashara katika Chuo Kikuu Mzumbe na kutembelea ofisi za shirika, pamoja na miradi inayotekelezwa na shirika ambayo ni HIV Prevention Care and Support, DREAMS na FOSENI II (Food Security and Nutrition Improvement) kwa lengo la kuona ni maeneno gani ambayo yanaweza kuboresha zaidi ushirika wa Chuo Kikuu cha Mzumbe na Shirika la Uwiano wa Maendeleo Vijijini. Katika ziara hiyo timu ya Chuo Kikuu cha Mzumbe ilieleza kua imejifunza mengi sana kwenye miradi inayotekelezwa na shirika na wameona maeneo mengi ambayo yanaweza kuboresha zaidi uhusiano ulipo kati ya shirika na Chuo Kikuu cha Mzumbe kama vile:- Kushauri na kusaidia kwa namna gani bidhaa zinazotengenezwa na wanufaika wa mradi wa DREAMS zifike sokoni vile vile kutoa msaada wa ...
Image
  Klabu ya Kupambana na Kudhibiti Ukatili wa Kijinsia na Watoto iliyopo katika shule ya sekondari Mwalimu Nyerere kata ya Chipaka, Halmashauri ya Mji Tunduma iliyoanzishwa na Shirika la IRDO kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Wilaya ya Momba Bahati Simchile - Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi na Mkuu wa Dawati la Jinsia na Haki za Watoto wilaya ya Momba akiwa na Judith Mwalukoba, Mshauri wa Mabinti na Rose Luvanda, Afisa Rasilimali Watu kutoka Shirika la Uwiano wa Maendeleo Vijijini (IRDO) wakitoa elimu na kushiriki michezo mbalimbali lengo ikiwa ni kupambana na kudhibiti ukatili wa kijinsia na kutetea haki za watoto kwenye Klabu ya Kupambana na Kudhibiti Ukatili wa Kijinsia na Watoto iliyopo katika shule ya sekondari Mwalimu Nyerere kata ya Chipaka, Halmashauri ya Mji Tunduma iliyoanzishwa na Shirika la IRDO kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Wilaya ya Momba inayowalenga watoto wa kike na kiume waliopo shuleni ili kuwasaidia kuelewa na kupambana dhidi ya ukatili wa kijinsia na...
Image
Mafunzo ya Uwezeshaji Kiuchumi kwa Wasichana Balehe na Wanawake Vijana Mafunzo ya Uwezeshaji Kiuchumi kwa Wasichana Balehe na Wanawake Vijana (wenye umri wa miaka 15 hadi 24) yaliyofanyika katika Kata ya Majengo, Halmashauri ya Mji wa Tunduma, Mkoa wa Songwe yaliyowezeshwa na IRDO kupitia mradi wa DREAMS kwa ufadhili wa HJFMRI. Katika mafunzo haya, washiriki walijifunza maarifa ya utengenezaji wa sabuni ya unga, mafuta ya mgando, na ubuyu ikiwa ni jitihada za kuboresha hali zao za kiuchumi kupitia fursa mbalimbali za ujasiriamali. Picha za tukio