Elimu kwa Jamii: Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nyerere Wapata Mafunzo Kuhusu Ukatili wa Kijinsia, UKIMWI, na Dawa za Kulevya
Katika jitihada za kuelimisha na kuhamasisha jamii kuhusu masuala muhimu ya kijamii na kiafya, Shirika la IRDO limefanya shughuli mbalimbali za kuelimisha wanafunzi. Shughuli hizi zilijumuisha igizo, shairi, na elimu ya moja kwa moja kutoka kwa wataalam.
Kwa upande mwingine, Bw. Johnson Samwel Bilingi, Mkaguzi Msaidizi wa Kituo cha Polisi Tunduma, aliongeza kwamba wanaume pia wanaweza kufanyiwa ukatili wa kijinsia na hawapaswi kusita kutoa taarifa. Aliwaasa wanafunzi kwamba ukatili unaweza kumtokea mtu yeyote bila kujali jinsia au umri, na ni muhimu kutoendelea kukaa kimya wanapoona vitendo vya ukatili mitaani.
Pia, wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nyerere walionesha igizo lenye ujumbe mzito kuhusu unyanyapaa dhidi ya watu wenye maambukizi ya Virusi vya UKIMWI. Igizo hili lililenga kuelimisha jamii kuhusu madhara ya unyanyapaa na kuhamasisha upendo na usawa kwa watu wote.
Aidha, wanafunzi hao walighani shairi kuhusu athari za dawa za kulevya kwa afya na jamii kwa ujumla. Ushairi huo ulilenga kutoa elimu na kuhamasisha kuhusu madhara ya matumizi ya dawa za kulevya.
Mwisho, Bw. Eliuthelius Lusungu, Community Change Agent kutoka shirika la IRDO ambae pia ni mnufaika wa mradi wa kuondoa uraibu wa dawa za kulevya (MAT), alitoa elimu kuhusu sheria zinazohusu kemikjinsi ya kupambana na changamoto hizo kwa maisha yao ya kila siku
IRDO|For Betteer Change
Comments
Post a Comment